FUKUNYUZI BLOG
KWA HABARI KEMKEM TOKA KILA KONA YA DUNIA
Sunday, April 26, 2015
Rais Kikwete kuongoza maadhimisho ya muungano
Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa leo anawaongoza Watanzania katika kuadhimisha miaka 51 ya kuzaliwa kwa Tanzania baada ya kuunganisha nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu umeasisiwa na mashujaa wa nchi hii ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume tarehe 26/4/1964. Muungano huo ulifanyika baada ya nchi hizi mbili kujipatia uhuru wake ambapo Tanganyika ilipata uhuru mwaka Desemba 1961 na Zanzibar Januari 1964. Katika sherehe hizo Watanzania watashuhudia matukio kadhaa yakiwemo ya kijeshi ambapo gwaride lililioandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama litapita kwa mwendo wa taratibu na mwendo wa kasi pamoja na ndege za kivika kupita huku zikionesha manjonjo yake katika kutoa heshima kwa rais Kikwete Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Mbali na hayo pia kutakuwa na halaiki ya watoto wakionesha mambo mbalimbali yanayohusiana na sherehe hii ya leo. Ndani ya miaka hiyo 51 mataifa hayo yamepiga hatua katika maendeleo makubwa tofauti na wakati zinaungana. Maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja, Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Thursday, April 16, 2015
Zitto Kabwe: ACT-Wazalendo ipo tayari kushirikiana na UKAWA Kunufaisha Wananchi na Si Kugawana Uongozi
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kimesema
kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la
kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.
Kutokana na hali hiyo, kimewahakikishia Watanzania kuwa ujio wa chama
hicho ni wa kuleta mageuzi ya kweli kwa taifa badala ya porojo kama
vyama vingine vinavyofanya.
Akihutubia wananchi jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Ukombozi, mjini Singida, Kiongozi wa
ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kuwa hivi sasa Taifa limekuwa na
shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha
malengo ya kukitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.
Alisema kutokana na hali hiyo, ni lazima Taifa lijengwe upya kwa
matumaini, ikiwamo kuhakikisha vyama vinakuwa na ushirikiano wa dhati
utakaoleta mageuzi ya kimfumo na uchumi kwa Watanzania wote.
“Kumekuwa na shauku ya wananchi kwa sisi kushirikiana na vyama vingine
vya siasa ili kufanikisha malengo yetu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi
kwa kuubomoa mfumo wa uchumi unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi
na tumeueleza mara kadhaa.
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama
na hili linathibitishwa na jina letu, Alliance na msimamo wetu kuhusu
mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi
na si ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi huyo wa ACT alisema chama chao hakina tatizo na kipo tayari
kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao,
ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kuunganisha nguvu
kukitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi
wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii
kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Subscribe to:
Posts (Atom)

